DKT. KIJAJI AKUTANA NA MENEJIMENTI YA WIZARA

………….

Na Sixmund Begashe, Dodoma

Waziri wa Maliasili na Utalii, Mheshimiwa Dkt. Ashatu Kijaji, amekutana na Menejimenti ya Wizara pamoja na wataalamu kutoka idara na vitengo mbalimbali vya Wizara hiyo, kwa lengo la kupokea taarifa za utekelezaji wa shughuli za Wizara na kujenga uelewa wa pamoja kuhusu maendeleo ya sekta ya uhifadhi na utalii nchini.

Kikao hicho kimehudhuriwa na Katibu Mkuu wa Wizara, Dkt. Hassan Abbasi, pamoja na Naibu Katibu Mkuu, Bw. Nkoba Mabula. Katika kikao hicho, Mhe. Dkt. Kijaji amewataka kuendelea kutoa huduma bora kwa wananchi kwa kuzingatia maadili, weledi na moyo wa kujituma.

Aidha, aliwasisitiza viongozi na watumishi wa Wizara kuhakikisha wanawahudumia wananchi kwa kuzingatia misingi ya “Utu na Kazi”, hususan katika kipindi hiki cha sherehe za mwishoni mwa mwaka.