Mbeya. Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya limesema litafanya misako ya doria za magari, pikipiki na kutumia wanyama kazi (mbwa), katika kuimarisha ulinzi sikukuu ya Krismasi sambamba na kutoa maelekezo ya wamiliki wa fukwe, kumbi za starehe.
Hayo yamebainishwa kwenye taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na jeshi hilo na kusainiwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Benjamin Kuzaga leo Jumanne Desemba 23,2025. Ambapo pia ameonya watu wasiokuwa na kibali kupiga milipuko ya fataki.
Kuzaga amesema wamejipanga kukabiliana na matukio ya uhalifu kwa kufanya doria za miguu, mbwa, magari na pikipiki katika kuelekea sikukuu za mwisho wa mwaka.
“Tumejipanga kukabiliana na matukio ya uhalifu kwa kufanya doria za aina mbalimbali sambamba na kulinda usalama katika Barabara Kuu ya Tanzania na Zambia (Tanzam),kwa kufanya ukaguzi wa magari kwenye vizuizi ,”amesema.
Amesema maeneo ambayo Polisi usalama barabarani wataweka kambi ni pamoja na Iwambi, Inyala, na Shamwengo sambamba na kutumia kifaa maalumu cha kupima ulevi kwa madereva.
“Tutatumia kifaa maalumu cha kupima kiwango cha ulevi kwa madereva wakiwamo wa ndani na masafa marefu ili kuzuia ajali zinazo sababishwa na uzembe,”amesema.
Katika hatua nyingine Kuzaga amewataka wananchi kuhakikisha wanaacha waangalizi kwenye makazi yao pindi wanapotoka kwenda kwenye nyumba za ibada siku ya mkesha wa sikukuu za mwisho wa mwaka.
“Licha ya ibada na kwenye mikesha mbalimbali ya nyakati za usiku ili kuepuka matukio ya uhalifu na kukumbusha wazazi kuwa walinzi wa watoto katika maeneo yenye mikusanyiko, “amesema.
Wakati huohuo ,Kamanda Kuzaga amepiga marufuku mtu yoyote kupiga au kulipia mlipuko wowotev(fataki),bila kuwa na kibali cha Jeshi la Polisi bali kwa wale wenye kibali pekee.
“Nionye na kupiga marufuku mtu yoyote asiye na kibali asijaribu kupiga au kulipua mlipuko wowote, lakini wenye kibali wazingatie masharti na vigezo vya usalama wa upigaji,”amesema.
Kuzaga amewataka wamiliki wa kumbi za starehe na fukwe kuhakikisha wanaweka walinzi binafsi maeneo ya ndani na nje hususani kwenye maegesho ya magari ili kudhibiti wahalifu.
“Lakini pia wajue uwezo wa kumbi zao kuchukua watu wangapi ili kuepuka kuzidisha na kusababisha madhara ya kibinadamu ikiwepo kukosekana kwa hewa ya kutosha,”amesema.
Pia amewataka wamiliki wa maeneo ya fukwe kama Matema na Ngonga Wilaya ya Kyela, na Kisiba -Ziwa Ngosi kuimarisha ulinzi na waangalizi kutokana msimu huu wa sikukuu kupokea watu rika tofauti ili kuepuka madhara.
Mkazi wa Jakalanda Mkoa wa Mbeya ,Salome John ameomba Serikali kudhibiti uhalifu kwa kufanya doria kwenye vilabu vya pombe ambako hujitokeza matukio mengi ya kudhuru
