Vatcan. Baba Mtakatifu Papa Leo XIV amesema Krismasi ya mwaka 2025 kuwa ni maalumu kwa ajili ya kutangaza na kuhubiri amani kwa sababu Yesu Kristo ndiye chimbuko la amani hiyo.
Papa Leo XIV katika salamu zake kwa Sherehe za mkesha wa Krismasi, amesema Sikukuu ya Noeli ni kwa ajili ya kutangaza na kuhubiri amani duniani kote.
Papa amehimiza Wakristo duniani kuishi kwa matumaini na hivyo kuendelea kuwa ni mashuhuda wa fadhila ya matumaini inayokita mizizi yake katika imani inayomwilishwa katika matendo ya huruma: kiroho na kimwili, kielelezo cha imani tendaji.
Hata hivyo, Papa Leo XIV ameongoza maadhimisho ya Sikukuu ya Krismasi katika Ibada ya Misa Takatifu kwenye Kanisa kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican leo Desemba 25, 2025.
Awali, amesisitiza kuwa Sikukuu ya Krismasi ni mwaliko wa kutangaza na kushuhudia amani, umoja, upendo na mshikamano wa udugu wa kibinadamu.
Hivyo amewataka Wakristo kuishi kwa matumaini na hivyo kuendelea kuwa mashuhuda wa katika imani inayomwakilisha Yesu Kristo katika matendo ya huruma: kiroho na kimwili.
“Noeli ni sherehe ya watakatifu na wadhambi wanaopaswa kutubu na kumwongokea Mungu; ni furaha ya wazima wanaowajibika kuwatunza na kuwahudumia wagonjwa; ni sherehe ya matajiri wanaopaswa kuonesha huruma, upendo na mshikamano kwa maskini” amesema.
Amesema ni wakati wa kujikita katika ukweli na uwazi; uaminifu na udumifu katika mambo msingi; kwa kusamehe na kusahau; kwa kujenga na kudumisha urafiki na udugu wa kibinadamu;
