SHEMDOE AWATAKA WALIOKWENDA KUSHEHEREKEA KRISMASI VIJIJINI KUNUNUA BIDHAA ZA WENYEJI

Na James Mwanamyoto – Dar es Salaam
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OWM–TAMISEMI) Mhe. Prof. Riziki Shemdoe amewahimiza wananchi waliosafiri kutoka mijini kwenda vijijini, kuhakikisha wananunua bidhaa huko huko vijijini ili kuleta tabasamu na kuongeza mzunguko wa fedha vijijini.
Prof. Shemdoe ametoa wito huo katika salaam zake za Krismasi alizotoa Disemba 24, 2025, mara baada ya ziara yake ya kikazi aliyoifanya kwenye Soko la Kariakoo jijini Dar. es Salaam.
“Ndugu Watanzania wenzangu ambao tumefanikiwa kwenda kusherehekea Sikukuu ya Noel vijijini kwetu, tuhakikishe tunanunua bidhaa zinazopatikana vijijini huko huko kwa wenyeji wetu, ili tuwaachie tabasamu na kuunga mkono azma ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuinua kipato cha Watanzania,” amesisitiza Prof. Shemdoe.