MWAKINYO AMCHAPA MNIGERIA KWA KO

NA EMMANUEL MBATILO, MICHUZI TV

BONDIA wa Kimataifa Mtanzania, Hassan Mwakinyo amefanikiwa kuibuka mshindi wa pambano lake dhidi ya mpinzani wake Mnigeria, Stanley Eribo katika raundi ya pili tu.


Katika pambano hilo lililopigwa katika dimba la Warehouse Masaki, Dar es Salaam ambako zimepigwa ngumi haswa, pambano ambalo lilikuwa la raundi 10 lakini kufikia raundi ya pili mnigeria huyo aliomba poo baada ya kupokea kichapo.

Mwakinyo amesema nidhamu ya mazoezi na kuheshimu mchezo ndio kunamfanya awe mshindi mara kwa mara katika mapambano yake.