Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene, amesema Serikali imeanza utekelezaji wa maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, yanayolenga kufanya mabadiliko makubwa ndani ya Jeshi la Polisi.
Amesema mabadiliko hayo yamekusudiwa kuboresha utendaji kazi na kurejesha uhusiano mzuri kati ya Polisi na wananchi, kwa kulibadili Jeshi hilo kutoka kwenye matumizi makubwa ya nguvu, na kulielekeza zaidi kwenye utoaji wa huduma na urekebishaji wa sheria, hususan katika namna ya kuwakamata watuhumiwa.
Simbachawene ameeleza hayo katika mahojiano maalumu, akibainisha pia kuwa wizara yake itayafanyia kazi maoni na mapendekezo ya Tume ya Kuangalia Jinsi ya Kuboresha Taasisi za Haki Jinai, iliyoongozwa na Mwenyekiti Jaji Mohamed Othman Chande, iliyoundwa na Rais Dkt. Samia mwezi Januari 2023.
Related
