RC MTANDA APEWA TUZO YA AMANI NA JMAT

…………..

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda leo Desemba 29, 2025 amepokea tuzo ya kulinda amani kutoka kwa jumuiya ya maridhiano ya amani Tanzania (JMAT) ikiwa ni sehemu ya kutambua mchango wake katika kuilinda amani kwa kipindi cha mwaka 2025.

Wakati akipokea tuzo hiyo Mhe. Mtanda amesema ujio wa JMAT ofisini kwake ni ishara nzuri ya kuonesha kuwa serikali ya Mkoa wa Mwanza pamoja na wananchi wake wameshiriki katika kuijenga na kuilinda amani ya taifa.

“Serikali ya Mkoa wa Mwanza tunashukuru sana kwa kutambua mchango wetu katika kuimarisha amani na niwashukuru wananchi wa Mkoa wa Mwanza kwa kuwa wasikivu”. Amesema Mhe. Mtanda.

Mhe. Mtanda ameendelea kwa kuwahakikishia JMAT kuwa wataendelea kupokea ushirikiano kutoka ofisini kwake haswa kuelekea katika maadhimisho ya siku maridhiano yatakayofanyika kitaifa kanda ya ziwa na Mkoa wa Mwanza ukiwa ndo Mkoa mwenyeji.

Naye Mkurugenzi wa idara ya usimamizi, uwajibikaji na mahusiano Bi. Leila Bhanji ametoa ombi kwa Mkuu wa Mkoa kuwa mlezi wa JMAT Mkoa wa Mwanza kwa kutambua umuhimu wa kazi zake pamoja na hekima zake za kutatua migogoro na changamoto.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa JMAT Mkoa wa Mwanza Sheikh. Musa Kalwanyi amesema malengo ya wao kukutana na Mkuu wa Mkoa ni kutambua mchango wake katika kudumisha na kuimarisha amani ya Mkoa.