WAZIRI wa Kilimo, Mhe. Daniel Godfrey Chongolo (Mb) amefanya mazungumzo na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Alexander Mkumbo (Mb) katika ofisi ndogo za Wizara hiyo tarehe 29 Desemba 2025, jijini Dar es Salaam.
Mazungumzo hayo yamelenga kujadili maeneo ya kipaumbele katika Sekta ya Kilimo na dhana ya kilimo biashara katika kuleta tija zaidi kwa wakulima, ikiwemo uongezaji wa ubanguaji wa Korosho kwa kutumia teknolojia ya kisasa. Hatua hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa mpango wa Serikali wa kuhakikisha zaidi ya asilimia 50 ya Korosho zinazalishwa nchini zinabanguliwa ndani ya nchi ifikapo mwaka 2030.
Eneo lingine lililojadiliwa katika mazungumzo hayo ni kuweka msukumo kwenye uzalishaji wa mazao yanayochangia upatikanaji wa uhakika wa mafuta ya kula nchini kama vile Michikichi na Alizeti, ili kupunguza na hatimae kutokomeza utegemezi wa mafuta yanayotoka nje ya nchi.
.jpeg)
