TAIFA STARS YAFUZU HATUA YA MTOANO AFCON

NA EMMANUEL MBATILO, MICHUZI TV

Timu ya Taifa ya Tanzania “Taifa Stars imefanikiwa kufuzu hatua ya mtoano ya michuano ya Kombe la Mataifa Afrika (AFCON) kwa mara ya kwanza kwenye historia tangu michuano hiyo ianzishwe mwaka 1957 baada ya kulazimisha sare ya 1-1 dhidi ya Tunisia.

Taifa Stars imefuzu hatua hiyo kwa njia ya “Best Loser” baada ya kumzidi Angola kwenye kigezo cha idadi ya mabao ya kufunga

Mchezo unaofuata katika hatua ya 16 bora Stars watakipiga dhidi ya Wenyeji wa michuano hii Timu ya Taifa ya Morocco.