Diwani wa kata ya Kalangalala Ruben Sagayika amewashika mkono wafungwa katika Gereza la wilaya ya Ya Geita kuelekea sikukuu ya mwaka mpya.
Sagayika ametoa zawadi mbalimbali Leo Disemba 31 2025 ikiwa ni sehemu ya kuwafanya wafugwa hao kujisikia ni sehemu ya jamii ya watu wa Geita.
Mkuu wa Gereza la Geita Jovin Bugwina amekili kupokea zawadi hizo kwa niaba ya wafungwa wa Gereza hilo na kutoa wito kwa wadau wengine kufata nyayo za diwani Sagayika.
Katika hatua nyingine diwani huyo ametoa zawadi kwa watoto Yatima wanaolelewa katika kituo Cha moyo wa huruma.
Msimamizi mkuu wa kituo Cha moyo wa huruma Sister Maria Lauda amemshukuru diwani kwa kuongeza tabasamu katika nyuso za watoto hao.


