MBUNGE CHATO AFICHUA ALIVYOTAPELIWA KEKUNDU KA PESAhi

………….

CHATO

KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida Mbunge wa Jimbo la Chato Kusini, Pascal Lukas Lutandula, amefichua jinsi alivyotapeliwa pesa za mama yake mzazi baada ya kucheza kamari ambayo ni maarufu kwa jina la kekundu ka pesa.

Pasipo kutaja kiwango cha fedha zilizoliwa katika mchezo huo, amewakubusha jinsi anavyozifahamu shida zao na jinsi alivyojiandaa kuzitatua hata kwa pesa zake binafsi ili wananchi hao wafurahie kuwa na kiongozi mwenye uchungu na maendeleo.

“Ndugu zangu wananchi wa Bwera ninawaahidi kuwa sitawaacha kamwe, mimi hapa ni nyumbani na bado huwa nakumbuka jinsi niliyokuwa nafanya biashara ndogo ndogo ya kuuza vitumbua, na sitosahau jinsi nilivyoliwa hapa hela za mama yangu kwenye mchezo wa kekundu ka pesa”

“Hata hivyo niwaeleze tu kuwa nimekuja hapa kwa mambo mawili, moja ni kuwashukuru sana kwa kunipigia kura nyingi zilizonipitisha kuwa Mbunge, pili nimekuja kuwatakia heri ya Krismasi na mwaka mpya wa 2026, na ili muweze kusherehekea kwa furaha leo ninawakabidhi ng’ombe mmoja, kg 250 za mchele, mafuta ya kupikia na kiasi cha shilingi 100,000 ili iwasaidie katika viungo vingine” amesema Lutandula.

Vile vile ameahidi kuwapatia vijana vifaa vya michezo ili kuibua vipaji vyao, kuimalisha afya pamoja na kupata burudani baada ya kumaliza kufanya kazi za uzalishaji mali.

Pia anakusudia kuandaa bonanza la michezo mbalimbali kwa mwakani 2026 ili wananchi wapate fursa ya kushuhudia na kushiriki burudani hizo zenye lengo la kuchochea uchumi wa mtu mmoja mmoja, vikundi na jamii kwa ujumla.

Awali Diwani wa kata ya Bwera, Josephat Manyenye, amemweleza Mbunge huyo changamo zinazowakabili wananchi wake ikiwemo ukosefu wa huduma ya Zahanati ambapo wagonjwa na wajawazito wanalazimika kutembea umbari mrefu.

Kadhalika ametumia fursa hiyo kuwashukuru wananchi hao kwa Imani kubwa waliyokipa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kumpigia kura za ushindi Rais Samia Suluhu Hassan, Mbunge na Diwani waliotokana na Chama hicho huku akiwasisitiza kuwa muda wa kampeni umekwisha na kinachopaswa sasa ni kufanya kazi kwa bidii.

Hata hivyo amewasihi kuendelea kuimalisha amani ya nchi kwa kuwa maendeleo yote yaliyoahidiwa hayawezi kutekelezeka iwapo nchi itakuwa kwenye machafuko.

Baadhi ya wananchi wa Bwera wameonyesha kufurahishwa na kitoweo cha ng’ombe na kwamba sasa wanaanza kuelewa falsafa ya KAZI na BATA aliyokuwa akiwaahidi wakati wa kampeni.

                            Mwisho.