TFF yazipiga rungu Tausi, Bunda Queens kwa kushindwa kufika uwanjani
SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limetoa adhabu ya kuwapokonya pointi tatu klabu za Bunda Queens na Tausi baada ya kushindwa kufika uwanjani kwenye mechi za kwanza za Ligi Kuu ya Wanawake msimu huu 2025-2026. TFF imethibitisha kuwa, timu hizo zilikiuka Kanuni ya 32 ya Ligi ya Wanawake (2025) baada ya kutofika kucheza mechi…