MFAMASIA MSD KIZIMBANI KWA WIZI DAWA NA VIFAA VYA HOSPITALI VYA BILIONI TISA
MFAMASIA Jackson Mahagi (39) amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na mashtaka ya wizi wa dawa na vifaa vya hospitali vyenye thamani ya Sh bilioni tisa mali ya MSD. Mahagi ambaye ni Mfamasia wa Halmashauri ya Wilaya ya Momba mkoani Songwe amesomewa mashtaka yake mahakamani hapo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Aaron Lyamuya…