ONGEA NA ANTI BETTIE: Nimechoka kudhalilishwa na mume wangu
Mume wangu nikikosea au akikasirika jambo ananisema mbele ya watoto sifurahii tabia hiyo, nifanye nini ili aache maana ananidhalilisha sana. Pole kwa unachopitia, si jambo dogo wala la kupuuzwa, unapodharauliwa mbele ya watoto wako. Kwa hili hata mimi nakuunga mkono hupaswi kulifumbia macho bali kulikemea maana linaondoa utu wako mbele ya watu unaopaswa kuwafunza tabia…