Wazazi Mara watakiwa kula ‘bata’, wakikumbuka kulipa ada
Musoma. Mkuu wa Mkoa wa Mara, Kanali Evans Mtambi, amewahimiza wakazi kusherehekea sikukuu za Krismasi na Mwaka Mpya kwa busara, huku wakizingatia kuweka akiba kwa ajili ya mahitaji ya Januari, ikiwemo ada za shule. Kanali Mtambi ametoa wito huo leo Jumatano, Desemba 24, mjini Musoma, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu hali ya usalama…