Migogoro ya kisiasa Afrika na nafasi ya AU, Jumuiya za kikanda dhidi ya nguvu za nje
Dar es Salaam. Afrika ni bara lenye historia ndefu ya mapambano ya ukombozi dhidi ya ukoloni, lakini pamoja na hatua zilizopigwa katika kujenga mshikamano wa kisiasa na kiuchumi, bado linaendelea kukumbwa na changamoto kubwa za kisiasa na kijeshi. Hali hii imeendelea kuwapo licha ya kuanzishwa kwa Umoja wa Afrika (AU) na jumuiya mbalimbali za kikanda…