SERIKALI KUANZISHA KITENGO MAALUM KUPOKEA MAONI YA WANANCHI SAA 24
Na. Mwandishi wetu – Rukwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano Mhe. Deus Sangu amesema Serikali itaanzisha kitengo maalum cha huduma kitakachofanya kazi kwa saa 24 chenye jukumu la kupokea, kusikiliza na kufanyia kazi maoni, mapendekezo pamoja na kero za wananchi. Kitengo hicho kitawezesha wananchi kuwasilisha changamoto zao moja…