Dosari zamweka huru aliyedaiwa kusafirisha kilo 172.3 za bangi

Arusha. Mahakama Kuu Divisheni ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, Masjala Ndogo ya Musoma, imemwachia huru Miriam Usire, aliyeshtakiwa kwa kosa la kusafirisha kilo 172.3 za bangi. Hukumu imetolewa na Jaji Monica Otaru, aliyesema ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka umeshindwa kuhalalisha hatia dhidi ya mshtakiwa kwani unaacha shaka. Jamhuri ilidai Oktoba 2, 2023, katika Kijiji…

Read More

‘Gen Z’ Moulay Mwanamfalme wa Morocco anayevuma mitandaoni

Fainali za Kombe la Mataifa Afrika (AFCON) 2025 zinaendelea nchini Morocco kwa mataifa 24 kushindania ubingwa unaoshikiliwa na Ivory Coast. Ufunguzi wa fainali hizo ulifanyika Desemba 21, 2025 huku ukiteka hisia za watu wengi si ndani ya Morocco pekee, bali hata waliokuwa mbali wakishuhudia kupitia matangazo ya moja kwa moja yaliyorushwa mubashara na vituo tofauti…

Read More

Tanzania ya watu wasomaji inawezekana

Dar es Salaam. Tanzania ni miongoni mwa nchi   zinazokabiliwa na changamoto kubwa ya kukosa utamaduni wa kujisomea. Pamoja na kwamba elimu ni moja ya nguzo kuu ya maendeleo, Watanzania wengi hawajaweka usomaji kuwa sehemu ya maisha yao ya kila siku. Kwa ujumla, tabia ya kusoma nchini imeendelea kudidimia kwa sababu mbalimbali, ikiwamo ukosefu wa miundombinu…

Read More

Mwanga mpya kwa mafundi wasio na vyeti

Dar es Salaam. Kila siku asubuhi katika maeneo mengi ya nchi,   sauti mbalimbali husikika ambazo mara chache hupewa heshima ya kitaifa.  Ni sauti za nyundo zikigonga mbao kwa ustahimilivu, sauti za mashine za kukata mbao zikilia kwa mwangwi wa kazi. Kwingine utaona cheche za mafundi wachomeleaji zikimulika anga la karakana ndogondogo, mashine za kushona nguo  zikizunguka…

Read More

Hujachelewa kumtafutia mtoto shule bora

​Desemba inapowadia, mitaa mingi nchini hukumbwa na taharuki ya kipekee. Ni msimu wa shamrashamra za sikukuu, lakini kwa mzazi mwenye mtoto anayezindua safari ya elimu au anayehama darasa, huu ni wakati wa “msukosuko wa machaguo.”  Ni kipindi ambacho ofisi za walimu wakuu hujaa wazazi wenye nyuso za wasiwasi, huku wengine wakizunguka na magari kutafuta mabango…

Read More

Matumaini mapya NHIF bima ya afya kwa wote

Dar es Salaam. Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) umebainisha kuwa upo tayari kuanza utekelezaji wa bima ya afya kwa wote ifikapo Januari Mosi, 2026, kufuatia maboresho ya mifumo, maandalizi ya kifedha na ushirikishwaji wa wadau mbalimbali. Hayo yamesemwa leo Jumatatu Desemba 22, 2025 na Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Dk Irene Isaka wakati…

Read More