Jalada aliyemjeruhi mumewe kwa kumkata uume latua NPS
Arusha. Jalada la mashtaka kuhusu tuhuma zinazomkabili Anna Melami anayedaiwa kumjeruhi mumewe kwa kumkata uume, limepelekwa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka (NPS) kwa hatua zaidi. Anna anatuhumiwa kumjeruhi mumewe, Baraka Melami (40), usiku wa Novemba 19,2025 walipokuwa wamelala nyumbani kwao katika Kijiji cha Olevolosi,Kata ya Kimnyaki wilayani Arumeru. Melami alidai usiku wa saa saba kasoro…