CAG aanza mkakati wa kitaifa kuwanoa madiwani wamo waandishi wa habari
Kibaha. Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), imeanza utekelezaji wa mkakati wa kitaifa wa kuwajengea uwezo madiwani na waandishi wa habari nchini, hatua inayolenga kuimarisha usimamizi wa miradi ya maendeleo na uwajibikaji wa matumizi ya fedha za umma katika halmashauri. Akizungumza kuhusu mkakati huo, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini…