Wanafunzi 686 wakatisha masomo CUoM sababu zatajwa
Mbeya. Imeelezwa kuwa jumla ya wanafunzi 686 wa Chuo Kikuu cha Kikatoliki cha Mbeya (CUoM), wameshindwa kuhitimu masomo yao kutokana na sababu mbalimbali zikiwamo za vifo, utoro na kushindwa kutimiza vigezo vya kitaaluma. Kauli hiyo imetolewa leo Jumatano, Desemba 17, 2025 na Kaimu Mkuu wa chuo hicho, Profesa Romuald Haule, wakati wa mahafali ya 10…