Bado Watatu – 30 | Mwanaspoti
NIKAMJIBU: “RAISA, akijua, urafiki hautakuwepo tena kwa sababu nilimficha ukweli; na isitoshe, huyo Shefa alikuwa rafiki yake sana.”“Sasa msubiri baba yako aje umueleze; usikie atakwambia nini.”“Baba utamueleza wewe. Mimi siwezi kumueleza.”“Basi msubiri. Aliniambia anakwenda benki. Pengine muda huu anarudi.”Wakati mama ananiambia hivyo, Raisa akanipigia simu. Nikaipokea.“Habari ya huko, shoga?” akanisalimia.“Nzuri. Umeamkaje?”“Nashukuru, kumekucha. Ndiyo, nakufuata —…