Wananchi wahimizwa kutumia mfumo kuwatambua mawakili feki

Shinyanga. Naibu Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga, Asha Mwetindwa amesema Mahakama imekuja na mfumo wa kielektroniki wa e-Wakili ili kuwatambua mawakili wanaotakiwa kufanya kazi hiyo, hivyo amewasihi wananchi kuutumia. Amesema mfumo huo, ambao una miaka mitatu sasa tangu kuanzishwa kwake, bado haujajulikana kwa wananchi, jambo linaloweza kuwasababishia usumbufu endapo watamtumia wakili…

Read More

Mawaziri wa Habari na Teknolojia Afrika kujadili utawala wa mtandao

Dar es Salaam. Mawaziri wa Afrika wanaoongoza wizara  kwenye masuala ya habari na teknolojia wanatarajiwa kukutana jijini Dar es Salaam, katika kongamano la Jukwaa la Utawala wa Mtandao Afrika (AfIGF) wakijadili mambo muhimu yanayohusu sera, matumizi, kanuni na mambo mengine yanayohusisha uchumi wa kidigitali. Kongamano hilo linalotarajiwa kuanza Mei 29 hadi 31, 2025 limetanguliwa na…

Read More

Uamuzi wa Dk Tulia kutimkia Uyole waacha mjadala Mbeya

Mbeya. Uamuzi wa Mbunge wa Mbeya Mjini, Dk Tulia Ackson kutangaza nia ya kugombea jimbo jipya la Uyole, umeibua hisia tofauti kwa wananchi, baadhi wakiunga mkono na wengine wakipinga huku wadau na wachambuzi wa siasa wakitoa kauli. Dk Tulia ambaye ameongoza Jimbo la Mbeya Mjini kwa miaka mitano, akichukua nafasi ya mtangulizi wake, Joseph Mbilinyi…

Read More

Fadlu aweka kila kitu wazi atakavyoikabili Berkane

KOCHA  wa Simba SC, Fadlu Davids, amesema kikosi kiko tayari kwa mechi ya fainali ya marudiano ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya RS Berkane huku akisisitiza kuwa wachezaji wameshajifunza kupitia maumivu ya dakika 20 za kwanza kule Morocco. Akizungumza na waandishi wa habari visiwani Zanzibar, Fadlu amesema: “Ndiyo, tulikuwa tumejiandaa kikamilifu kwa mechi ya…

Read More

CCM KUZINDUA ILANI YA UCHAGUZI

::::::: Katibu wa itikadi na uenezi wa Cha Mapinduzi(CCM), CPA Amos Makalla amesema Chama hicho kinatarajia kufanya mkutano Mkuu Mei 29-30 ukitangaliwa na Kamati kuu(CC) na Halmashauri kuu(NEC). Amesema mkutano huo ambao maandalizi yake yameshakamili utakuwa na ajenda kuu tatu  ambazo ametaja kuwa ni kupokea taarifa ya utekelezaji Ilani CCM katika kipindi cha miaka mitano…

Read More

DPP alivyowang’ang’ania walioachiwa huru kwa mauaji Zanzibar

Zanzibar. Mahakama ya Rufani Zanzibar imebatilisha uamuzi wa kuwaachia huru washtakiwa watatu waliokuwa wakikabiliwa na mashtaka ya kuua na badala yake, imewaona wana kesi ya kujibu, hivyo kutakiwa kujitetea kortini. Watuhumiwa hao walikuwa wamefunguliwa shtaka la mauaji ya kukusudia kuwa Januari 17, 2017 saa 3:00 asubuhi, huko eneo la Tumbe Magogoni, Chakechake Pemba, walimshambulia na…

Read More