Mbunge adai kufanyiwa figisu asirudi bungeni
Dodoma. Homa uchaguzi mkuu wa Oktoba, 2025 imezidi kutanda ndani ya Bunge baada ya Mbunge wa Kyerwa (CCM), Innocent Bilakwate kudai kuwa kuna kiongozi anahonga pesa kwa mabalozi ili asichaguliwe. Amesema hatua ya kiongozi huyo ambaye pia ni mfanyabiashara wa kahawa imekuja baada ya Bilakwate kupambania maboresho ya bei ya kahawa. Uchaguzi mkuu wa Rais,…