Chadema Mbeya yavunja kambi ya kumsaka Mdude
Mbeya. Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimevunja rasmi kambi iliyokuwa imewekwa kushinikiza kupatikana kwa kada wao, Mdude Nyagali, huku kikieleza msimamo wao katika ushiriki wa uchaguzi mkuu na uzinduzi wa kampeni ya ‘No reforms, no election’ mkoani Mbeya. Pia kimewataka wananchi na wafuasi wao kupuuza taarifa za baadhi ya waliojivua uanachama wa chama hicho,…