2025
Mwembe Makumbi yarejea kileleni, Mlandege ikifanya mauaji ZPL
TIMU ya Mwembe Makumbi City, imerejea kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu Zanzibar (ZPL) baada ya kuitandika Chipukizi bao 1-0 katika mchezo uliofanyika leo Jumapili Mei 18,2025 kwenye Uwanja wa Finya uliopo kisiwani Pemba. Mwembe Makumbi ambayo ilikaa kileleni kwa takribani miezi minne kabla ya kushushwa na Mafunzo hatimaye, imerejea katika nafasi hiyo baada ya…
Yanga yamuuza rasmi Aziz KI, acheza mechi ya mwisho
Kama umemuona kiungo Stephanie Aziz KI uwanjani leo akiichezea Yanga basi umebahatika kumtazama kwa mara ya mwisho kiungo huyo akiwa na jezi ya timu hiyo. Yanga leo Jumapili imemuaga rasmi kiungo huyo uwanjani na wakati wowote kuanzia sasa atatimka kwenda kujiunga na klabu mpya huko Afrika Kaskazini. Taarifa ya uhakika ni kwamba, Yanga itamuuza Aziz…
Maafa mgodini | Mwananchi
Shinyanga. Kuporomoka kwa kifusi katika mgodi unaomilikiwa na kikundi cha Hapa Kazi Tu, Mwakityolo mkoani Shinyanga, kumepoka uhai wa watu sita na kuwajeruhi 17 kwa mujibu wa taarifa rasmi ya uokozi hadi leo saa 12:00 jioni. Hadi taarifa ya mwisho ya uokozi ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoani Shinyanga inayotolewa leo, inadaiwa watu 20…
Watatu wahukumiwa miaka 30, jela kila mmoja kwa ubakaji
Mbeya. Watu watatu wakazi wa wilaya za Chunya na Mbarali mkoani Mbeya wamehukumiwa kutumikia kifungo cha miaka 30 jela kila mmoja baada ya kupatikana na makosa ya ubakaji. Katika tukio la kwanza, Mahakama ya Wilaya ya Mbarali mkoani hapa, imemuhukumu Kulwa Memba (30), mkazi wa Kijiji cha Lukali kutumikia kifungo cha miaka 30 jela baada…
CCM yatia neno barua ya msajili kwa Chadema, chajibu
Bukoba. Chama cha Mapinduzi (CCM) kimesema hatua ya Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, kukiamuru Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kuitisha upya Baraza kuu ili kuziba nafasi ya wajumbe wanane, chama hicho kisitafute mchawi bali wao ndio wenye makosa. Kauli hiyo ya CCM, imetolewa na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho,…
Changamoto tishio sekta ya nyuki zatajwa
Dodoma. Mambo manne yametajwa kutishia uendelevu wa sekta ya nyuki nchini Tanzania, ikiwemo matumizi ya dawa za kuua wadudu katika kilimo yasiyozingatia kiwango kinachotakiwa. Mambo mengine ni ubadilishaji wa matumizi ya misitu kwa ajili ya shughuli nyingine, uchomaji wa misitu na mabadiliko ya tabianchi. Hayo yamebainishwa leo Mei 18, 2025, na Mkuu wa Mkoa wa…
Kilichompa ushindi Profesa Janabi, Tanzania itakavyonufaika
Dar es Salaam. Ukiachana na uwezo wake kiuongozi na hotuba yake iliyoakisi kiu kubwa ya Waafrika, sifa ya Tanzania kidiplomasia barani Afrika ni miongoni mwa mambo yaliyochangia ushindi wa Mkurugenzi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Kanda ya Afrika, Profesa Mohamed Janabi. Kipindi cha kampeni iliyochukua takribani miezi mitatu, Mjumbe Maalum wa Rais Samia Suluhu…
CG MWENDA HAPOI, ATEMBELEA KIWANDA CHA SIGARA TCC PLC
::::::: Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Yusuph Juma Mwenda amefanya ziara katika kiwanda cha Sigara Tanzania cha TCC PLC Jijini Dar es Salaam Mei 17.2025 na kujiridhisha kwamba uzalishaji unaofanyika unaendana na kiwango cha Kodi inayolipwa na kiwanda hicho. Akiwa kiwandani hapo Kamishna Mkuu ametembelea maeneo ya…
WIZARA YA MIFUGO NA UVUVI YAZINDUA MAFUNZO YA WATAALAM WA AFYA YA MIFUGO
Wizara ya Mifugo na Uvuvi imezindua rasmi mradi wa mafunzo kwa wataalamu wa mstari wa mbele wa afya ya mifugo, yanayofanyika katika nchi nne: Tanzania, Botswana, Zambia na Malawi. Akizungumza leo Mei 17, 2025 katika Chuo cha LITA, Kampasi ya Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Profesa Riziki Shemdoe, amesema kuwa mafunzo hayo…