CCM yapigilia msumari hoja ya Rais Samia kuhusu wanaharakati
Geita. Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Amos Makalla amesema Tanzania ni nchi huru yenye mamlaka kamili, hivyo ina uwezo wa kuamuru mgeni gani aingie nchini na nani asiingie. “Nimeona kwenye mitandao ya kijamii, oooh oooh… mara wanaharakati mara kina Martha Karua na wenzake wamezuiwa uwanja wa ndege walikuwa wanakuja…