Wanahisa CRDB waidhinisha gawio la kihistoria la Sh170 bilioni
Arusha. Wanahisa wa Benki ya CRDB Plc wameidhinisha kwa kauli moja gawio la jumla la Sh170 bilioni, ambalo ni kubwa zaidi kuwahi kutolewa na benki hiyo. Hilo limejiri katika mkutano mkuu wa mwaka wa 30 (AGM) uliofanyika jijini Arusha mwishoni mwa wiki. Gawio hilo linaloidhinishwa lina maana ya Sh65 kwa kila hisa kwa wanahisa wa…