Wahamiaji haramu 35 wakamatwa K’njaro wakiwa shamba la mahindi
Moshi. Wahamiaji haramu 35 raia wa Ethiopia na Burundi wamekamatwa Mkoa wa Kilimanjaro wakitumia njia za panya (njia zisizo rasmi) kuingia nchini Tanzania kinyume cha sheria. Wahamiaji hao wamekamatwa Mei 10 na Mei 15, 2025 katika Kijiji cha Mji Mpya kata ya Mabogini, Wilaya ya Moshi mkoani humo baada ya maofisa wa Uhamiaji kupata taarifa…