KVZ yaizima Malindi, ikiingia vita ya ubingwa
MAAFANDE wa KVZ jana imeizima Malindi kwa mabao 2-1 na kuchupa hadi nafasi ya pili kutoka ya nne ikiingia katika vita ya ubingwa wa Ligi Kuu Zanzibar (ZPL). Ushindi huo uliopatikana kwenye Uwanja wa Mao A umeifanya KVZ kufikisha pointi 47, moja pungufu na ilizonazo Mafunzo inayoongoza msimamo ambayo nayo jana ilibanwa mbavu na Zimamoto…