Bazecha watoa msimamo mtikisiko wa kisiasa Chadema

Dar es Salaam. Baraza la Wazee la Chadema (Bazecha) limesema licha ya hamahama ya baadhi ya viongozi na wanachama wa chama hicho, uimara wa Chadema sasa ni mkubwa kuliko wakati mwingine wowote. Baraza hilo limetafsiri hatua ya baadhi ya makada wa chama kujivua nyadhifa zao na kuondoka kama hatua mojawapo inayopitiwa na bahari kutema uchafu….

Read More

Tanzania yajipanga, WHO ikipunguza idara, watumishi

Dar es Salaam. Wakati Shirika la Afya Duniani (WHO) likipunguza idara zake kutoka 76 hadi 34 na gharama za wafanyakazi kwa asilimia 25 baada ya ufadhili kupungua, Tanzania imeanza kujipanga kukabiliana na hatua hiyo. WHO imechukua hatua hiyo ikiwa takribani miezi minne baada ya Marekani kutangaza kujiondoa katika shirika hilo na kusitisha ufadhili wake. Mkurugenzi…

Read More

Wananchi wa Dumila, Kilosa wambebesha ‘zigo’ Makalla

Morogoro. Wananchi wa Dumila, Wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro wamesema upatikanaji wa maji safi na stakabadhi ghalani, barabara za ndani ni miongoni mwa kero zinazowasumbua, hivyo wamemuomba Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Amos Makalla kuingilia kati. Hata hivyo, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Adam Malima amewajibu kuwa tatizo la…

Read More

Nauli elekezi kwa bodaboda ni vuta nikuvute kwa madereva, abiria

Unguja. Siku moja baada ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) kutangaza iko katika hatua za mwisho kuandaa nauli elekezi kwa waendesha bodaboda, baadhi ya madereva wa vyombo hivyo wameomba viwango hivyo vizingatie umbali wa safari, wakisisitiza huduma wanazotoa hazifuati njia maalumu (ruti) kama ilivyo kwa daladala. Wakati waendesha bodaboda wakitaka upangaji wa nauli uzingatie…

Read More

Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Dodoma ajivua uanachama

Dodoma. Mwenyekiti wa Chama cha Maendeleo na Demokrasia (Chadema) Mkoa wa Dodoma, Aisha Madoga amejiengua uanachama wa chama hicho. Uamuzi huo wa Madoga kukihama chama umefanyika leo Mei 16,2025 jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari. Miongoni mwa sababu alizoeleza kujivua uanachama na kuacha madaraka yake ndani ya chama hicho ni kutokuwa na uhuru…

Read More

DK.ANGELA NANYARO AELEZEA ATHARI YA MNYORORO WA HUDUMA KWA MAMA

Na Mwandishi Wetu Afya ya mama ni msingi wa jamii yenye afya. Tunapowatunza wakina mama, tunaziimarisha familia, jamii, na vizazi vijavyo. Kusaidia afya ya mama kunamaanisha kuhakikisha wanawake wanapatahuduma bora kabla, wakati, na baada ya kujifungua. Yaani mnyororo wa huduma unaolinda maisha yamama na mtoto. Kabla ya kujifungua, upatikanaji wa huduma za klinikiza wajawazito husaidia…

Read More