Wananchi kupata huduma za madini mahali pamoja
Dodoma. Changamoto ya wananchi kusumbuka kuzunguka maeneo mbalimbali kutafuta huduma za Wizara ya Madini imekwisha, baada ya wizara hiyo kukamilisha ujenzi wa jengo la makao makuu lililopo Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma, na kuhamia rasmi. Kuhamia katika jengo hilo ni utekelezaji wa ahadi aliyotoa Waziri wa Madini, Anthony Mavunde, Machi 20, 2025, wakati Kamati…