Mwita: Ninaijua Kibamba, nitashughulikia changamoto zilizopo
Dar es Salaam. Mgombea udiwani kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Kibamba, Otaigo Mwita, amesema amedhamiria kutatua changamoto zilizopo katani humo atakapopewa ridhaa na wananchi katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025. Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni zake leo Septemba 12, 2025 eneo la Kibamba Shule, amesema anaielewa vizuri hali ya kata hiyo…