Wadau wa utalii wahimizwa kutoa ushauri wa kuboresha sekta hiyo
Dodoma. Serikali imewataka wadau wa utalii nchini kufunguka kwa kutoa ushauri wa jinsi ya kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji katika sekta ya utalii. Hayo yamebainishwa leo Jumanne Mei 13, 2025 na Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Pindi Chana wakati wa mkutano wa nne wa majadiliano kati ya wadau wa utalii na wizara yake….