NIKWAMBIE MAMA: Hivi wote tunakijua tunacho kichagua?
Watanzania ni watu wanaohitaji elimu kila sekunde. Huwa wanafurahishwa bila kujua kinachowafurahisha, na wakati mwingine wanachukizwa bila kulijua chukizo lao. Wanaweza kuingia taabuni kutokana na watu wabaya wanaowazunguka, lakini wakawa tayari kuwalinda watu hao wawe ni ndugu au wahamiaji haramu. Inawezekana maisha ya kidugu waliyozoeshwa ndiyo sababu ya tabu zao. Ni watu wasiopenda kujifunza kutokana…