KONA YA MALOTO: Lenzi ya G55 Chadema imekosea hisabati kisiasa
Walianza kwa kuandika barua, kisha wakatoka na kuzungumza na vyombo vya habari. Walidai kwamba msingi wa wao kutoka hadharani ni baada ya Mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu, kudonyoa baadhi ya hoja za barua yao na kuzijibu hadharani. Mambo mengi yanayozungumzwa ni kinogesho tu. Chanzo kikuu cha mtafaruku ni msimamo wa uongozi wa juu wa chama…