MIAKA 20 GEREZANI KWA KUHUJUMU MRADI WA ETDCO

Na Mwandishi Wetu  MAHAKAMA ya Wilaya ya Lugoba, Halmashauri ya Chalinze Mkoani Pwani, imewahukumu watu wawili, Mayunga Senteu na Muganyi Makulu, kifungo cha miaka 20 jela kila mmoja baada ya kupatikana na hatia ya kuiba na kuharibu miundombinu ya umeme. Wawili hao walikutwa na hatia ya kuiba nyaya za umeme aina ya ACSR kutoka katika…

Read More

ULEGA AVUNJA MKATABA WA MKANDARASI MZEMBE

 :::::::::: Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega ametangaza kuvunjwa kwa mkataba wa ujenzi wa barabara Mkoani Tanga baada ya Mkandarasi kutoka China kushindwa kutimiza masharti ya mkataba.  Mkandarasi huyo, kampuni ya China Railway 15 Bureua Group anayejenga barabara ya Tanga – Pangani – Mkwaja – Bagamoyo (Makurunge) sehemu ya Tungamaa – Mkwaja – Mkange (km 95.2)…

Read More

IAA YAANZA UJENZI KAMPASI YA SONGEA

SHILINGI Bilioni 18, zimetolewa kupitia Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET), ili kufanikisha ujenzi Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) kampasi ya Songea. Hayo yameelezwa na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Mheshimiwa Kanali Ahmed Abbas wakati wa hafla ya makabidhiano ya eneo la ujenzi wa IAA kampasi ya Songea kwa Mkandarasi. Kanali…

Read More

‘Muwaamini makandarasi wazawa, wapeni mikopo’

Njombe. Taasisi za kifedha nchini zimeshauriwa kuwaamini na kuwapa kipaumbele wakandarasi wazawa kwa kuwapatia mikopo, ili watekeleze miradi ya Serikali kwa ufanisi na kwa wakati, bila vikwazo vya kifedha. Wito huo umetolewa leo, Jumatatu Mei 12, 2025 na Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Anthony Mtaka, wakati wa hafla ya kusaini mkataba wa ujenzi wa majengo…

Read More

Mikopo ya elimu ya juu yaongezeka

Dodoma. Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imewasilisha vipaumbele vitano itakavyotekeleza katika mwaka wa fedha wa  2025/2026,  huku idadi ya wanufaika wa mikopo ya elimu ya juu ikitarajiwa kuongezeka kutoka 245,314 mwaka 2024/2025 hadi wanafunzi 252,773 mwaka ujao wa fedha. Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda ameyasema hayo leo Jumatatu Mei 12,2025…

Read More

Mvua yakata mawasiliano barabara ya Ifakara–Mlimba

Mlimba. Mvua kubwa iliyonyesha usiku wa kuamkia leo huko Mlimba imesababisha kukatika kwa barabara ya Ifakara–Mlimba kwenye maeneo mawili, hivyo kukata mawasiliano wilayani humo. Barabara hiyo imekatika kwenye eneo la Kijiji cha Ngwasi na Kalengakelu, Halmashauri ya Mlimba, na kwamba mvua kubwa inayoendelea kunyesha wilayani humo imesababisha maeneo mengi kuharibika. Akizungumza na Mwananchi, Diwani wa…

Read More

Alichozungumza Papa Leo XIV na Zelensky

Vatican. Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki, Papa Leo XIV amefanya mazungumzo ya simu na Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky ikiwa ni simu ya kwanza kuzungumza na kiongozi wa kitaifa tangu achaguliwe katika wadhifa huo. Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika leo Jumatatu Mei 12, 2025, Papa Leo na Zelensky wamezungumzia mapendekezo ya usitishaji mapigano na malumbano kati…

Read More

Mangi Marealle akimbilia Mahakama Kuu

Moshi. Mfanyabiashara mashuhuri na Mangi wa Wachaga wa Marangu mkoani Kilimanjaro, Frank Marealle ameanzisha mchakato wa rufaa kupinga hukumu ya Baraza la Ardhi na Nyumba Moshi, lililokataa maombi yake aliyoyafungua mwaka 2020. Marealle aliomba Baraza litoe amri kwamba ardhi yenye mgogoro ni mali yake na ya kufukuliwa kwa kaburi na kuondoa jeneza lenye mwili wa…

Read More