‘Lenacapavir’ dawa iliyoonyesha ufanisi kuzuia VVU kwa asilimia 100
Dar es Salaam. Dawa ya sindano aina ya lenacapavir inayozuia maambukizi ya virusi vya Ukimwi, imeonyesha ufanisi kwa asilimia 100 katika jaribio la kwanza la utafiti nchini Uganda. Iwapo lenacapavir itaidhinishwa, inaweza kubadili kabisa mikakati ya kuzuia VVU duniani. Lengo la utafiti huo lilikuwa ni kutafuta suluhu ya changamoto katika matumizi, ufuasi na kudumu katika…