Wafanyabiashara Iringa wafunga maduka, wananchi wahaha
Iringa. Wananchi wa Mkoa wa Iringa wamejikuta katika hali ya taharuki na usumbufu, kufuatia kufungwa kwa biashara nyingi katikati ya mji kuanzia asubuhi ya leo, Mei 12, 2025. Tukio hilo limeathiri upatikanaji wa huduma na bidhaa muhimu kwa wakazi wa Iringa, ambao kwa kawaida hutegemea sana biashara za mjini kwa mahitaji yao ya kila siku….