Mvua yakata mawasiliano barabara ya Ifakara–Mlimba
Mlimba. Mvua kubwa iliyonyesha usiku wa kuamkia leo huko Mlimba imesababisha kukatika kwa barabara ya Ifakara–Mlimba kwenye maeneo mawili, hivyo kukata mawasiliano wilayani humo. Barabara hiyo imekatika kwenye eneo la Kijiji cha Ngwasi na Kalengakelu, Halmashauri ya Mlimba, na kwamba mvua kubwa inayoendelea kunyesha wilayani humo imesababisha maeneo mengi kuharibika. Akizungumza na Mwananchi, Diwani wa…