Charles Hilary kuzikwa Zanzibar Mei 14, hii hapa ratiba kamili

Unguja. Mwili wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu na Msemaji Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) unatarajiwa kuzikwa Jumatano Mei 14, 2025 katika makaburi ya Mwanakwerekwe Zanzibar. Katika ratiba ya serikali iliyotolewa na kitengo cha Mawasiliano ya Rais Ikulu Zanzibar, mwili wa marehemu utatolewa katika hospitali ya Mloganzila na kupelekwa nyumbani…

Read More

ETDCO yakabidhiwa mradi, kuunganisha umeme vitongoji 105

Mbeya. Kampuni ya Ujenzi na Ukarabati wa Miundombinu ya Usafirishaji na Usambazaji wa Umeme (ETDCO), imekabidhiwa rasmi mradi wa kuunganisha umeme katika vitongoji 105 mkoani Mbeya. Mradi huo wenye thamani ya Sh10.9 bilioni umetekelezwa kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA), utanufaisha wateja takriban 3,465. Akizungumza katika hafla ya makabidhiano ya mradi huo iliyofanyika leo Kata…

Read More

BONANZA LA MAADHIMISHO YA WIKI YA USHIRIKA LAFANYIKA DODOMA,LATIA FORA

Mwenyekiti wa Jukwaa la Ushirika Mkoa wa Dodoma,Ibrahim Sumbe,akizungumza na waandishi wa habari wakati wa Bonanza la Ushirika kuelekea Siku ya kuelekea Jukwa la Ushirika Mkoa wa Dodoma linalotarajia kufanyika Mei 15-16,mwaka huu katika Ukumbi wa Chimwaga uliopo katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM),Bonanza lililofanyika leo Mei 10,2025 katika Viwanja wa Kilimani Jijini Dodoma. ………

Read More

Polisi yarejea Ligi Kuu Zanzibar 

Licha ya vita vya ngumi na midomo iliyotokea leo Jumapili katika mechi ya jasho na damu, maafande wa Polisi wameichakaza Kundemba kwa kuitandika mabao 3-1 kwenye  Uwanja wa Mao B, Mjini Unguja na msimu ujao watacheza Ligi Kuu Zanzibar. Timu nyingine zilizotinga ZPL kwa msimu ujao ni; New King, Fufuni na Wawi. Mechi hiyo iliyokuwa na…

Read More

NMB yanyakua tuzo sita kimataifa, Zaipuna anena

Dar es Salaam. Benki ya NMB imeendelea kutanua sifa na kutangaza huduma zake kimataifa kwa kupata ushindi wa kihistoria kwa kushinda tuzo sita za kimataifa kutoka kwa majarida mawili mashuhuri duniani; Euromoney, linalochapishwa jijini London, Uingereza, na Global Banking & Finance Magazine lenye makao makuu yake New Jersey, Marekani. Ushindi huo unaashiria kutambuliwa kwa ubora…

Read More

Mhandisi Mativila aridhishwa Utekelezaji wa Miradi ya Barabara ya Mtili-Ifwagi na Sawala-Iyegeya

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, TAMISEMI anayeshughulikia Miundombinu, Mhandisi Rogatus Mativila ametembelea na kukagua miradi ya ujenzi wa barabara za Mtili–Ifwagi na Sawala-Iyegeya, ambapo ameonesha kuridhishwa na miradi hiyo. Barabara hizo zinazojengwa na TARURA kwa lengo la kurahisisha usafirishaji wa mazao ya chai, misitu, mbogamboga na mazao mengine kufika sokoni kwa  wakati. Amesisitiza kuwa…

Read More

RAIS MWINYI AIFARIJI FAMILIA YA MAREHEMU CHARLES HILLARY

………… Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ametoa mkono wa pole kwa familia ya marehemu Charles Hillary, aliyekuwa Msemaji Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, aliyefariki dunia usiku wa kuamkia leo, tarehe 11 Mei 2025, jijini Dar es Salaam. Rais Dkt….

Read More