Mafunzo yaing’oa Mwembe Makumbi kileleni ZPL baada ya miezi mitatu
MAAFANDE wa Mafunzo imetwaa usukani wa Ligi Kuu Zanzibar (ZPL) baada ya kuibamiza Uhamiaji bao 1-0, kwenye Uwanja wa Mao B, mjini Unguja. Mafunzo iliyocheza mechi 24 kwa sasa imefikisha pointi 47, moja zaidi na ilizonazo waliokuwa vinara wa ZPL Mwembe Makumbi yenye pointi 46 iliyocheza mechi 23. Maafande hao sasa wamebakiwa na mechi sita…