2025
Ndoa ya Mserbia, KenGold yafikia tamati
KLABU ya KenGold imefikia uamuzi wa kuachana na aliyekuwa kocha wa timu hiyo raia wa Serbia, Vladislav Heric baada ya kikosi hicho cha Chunya mkoani Mbeya kushuka Ligi Kuu Bara kikiwa na mechi tatu mkononi za kuhitimisha msimu huu.
Serikali yaja na mwarobaini kuporomoka majengo
Dodoma. Wizara ya Ujenzi imewasilisha bajeti yake kwa mwaka 2025/26 huku ikisema kutokana na kuporomoka kwa jengo la ghorofa nne Kariakoo jijini Dar es Salaam inatunga sheria ya majengo kwa ajili ya kusimamia sekta ndogo ya majengo nchini. Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega ameyasema hayo leo Jumatatu Mei 5, 2025 wakati akiwasilisha makadirio ya mapato…
RAIS SAMIA ALIPA BIL 539 UKAMILISHAJI DARAJA LA JP MAGUFULI, MRADI WAKAMILIKA ASILIMIA 99
Wakati Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan akiingia madarakani mwaka 2021, ujenzi wa daraja la JP Magufuli (Kigongo – Busisi) mkoani Mwanza ulikuwa umefikia takribani asilimia 25 na kutokana changamoto za kutetereka kwa uchumi wa dunia baada ya janga la Uviko 19, hivyo kuwa na wasiwasi wa upatikanaji wa fedha. Hata hivyo serikali amekamilisha malipo…
RWEBANGIRA ATEMBELEA VITUO VYA KUPIGIA KURA CHUNYA MKOANI MBEYA
Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe.Magdalena K.Rwebangira ametembelea na kukagua vituo vya kuandikishia wapiga Kura vilivyo katika Halmashauri ya wilaya ya Chunya mkoani Mbeya ikiwa ni siku ya nne tangu kuanza kwa zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura awamu ya pili, mzunguko wa kwanza na uwekaji wazi wa…
Mbungi la fainali CAFCC kupigwa Kwa Mkapa, Mwana FA athibitisha
Zimebaki siku 20 tu kwa wakazi wa Dar es Salaam kuliona kombe la Shirikisho katika Uwanja wa Benjamin Mkapa Mei 25,2025 baada ya kuhakikishiwa na Serikali kuwa mechi ya marudiano ya fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika itachezwa katika uwwnja huo. Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hamisi Mwinjuma ameondoa ombwe lililokuwepo juu…
TANZANIA YAWAKILISHWA VEMA KWENYE KAMBI YA MAFUNZO YA HUAWEI SHENZHEN (CHINA)
Na Mwandishi wetu WANAFUNZI wenye vipaji katika sekta ya teknolojia ya habari na mawasiliano kutoka vyuo vikuu 12 duniani, wameshiriki katika kambi ya mafunzo ya kimataifa ya Huawei Global Seeds for the Future, iliyofanyika kuanzia Aprili 9 hadi Aprili 17, 2025 katika makao makuu ya Huawei huko Shenzhen nchini China. Kambi hiyo ya…
Nne Mbeya City zampa heshima Malale
KOCHA wa Mbeya City, Malale Hamsini ameandika rekodi nyingine kwa kuipandisha timu Ligi Kuu Bara msimu ujao, ikiwa ni kwa mara ya pili tangu afanye hivyo msimu wa 2022-2023, akiwa na kikosi cha maafande wa JKT Tanzania.
Mastaa hawa kuamua dabi | Mwanaspoti
ZIMESALIA siku mbili kabla ya kushuhudia mtanange wa Dabi ya Dar es Salaam kati ya JKT Queens na Simba Queens kwenye Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo jumatano hii. Timu zote ziko nafasi nzuri ya kutwaa ubingwa wa Ligi ya Wanawake unaotetewa na Simba. JKT iko kileleni na pointi 38 tofauti ya pointi moja na Simba…
Ngorongoro ina dakika 90 za uamuzi AFCON-U20
BAADA ya timu ya taifa ya vijana, Ngorongoro Heroes kupoteza mechi mbili za awali za Kundi A katika vita ya kuwania ubingwa wa Afrika (AFCON-U20), kwa sasa timu hiuo ina dakika 90 za kufufua tumaini la kuvuka hatua hiyo kwenda hatua inayofuata kusaka tiketi ya fainali za Kombe la Dunia 2025. Ngorongoro imesaliwa na mechi…