Chadema yamvua uanachama Mrema, mwenywe ajibu

Dar es Salaam. Wakati Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), tawi la Bonyokwa likitangaza kumvua uanachama John Mrema, kwa tuhuma mbalimbali ikiwemo ukaidi, mwenyewe amekana kufukuzwa uanachama. Tuhuma zingine anazodaiwa Mrema aliyewahi kuwa Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa chama hicho, sababu nyingine zilizotajwa ni pamoja na dharau dhidi ya mamlaka, kutoheshimu…

Read More

AG awajibu wanaokosoa utaratibu uliotumika kesi ya Lissu

Dodoma. Bunge limepitisha bajeti ya Wizara ya Katiba na Sheria kwa mwaka 2025/26 huku Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Hamza Johari amesema utaratibu wa kusikiliza kesi ya Mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu kwa njia ya mtandao ulifanywa kwa mujibu wa kisheria baada ya kufanya tathmini. Aprili 24,2025, Lissu alipinga kesi yake ya kuchapisha taarifa za…

Read More

Vijana wanaopenda ‘mashangazi’ kuna ujumbe wenu hapa

‎Iringa. Vijana mkoani hapa wametakiwa kuachana na tabia ya kutegemea mahusiano ya kimapenzi kama njia ya kupata unafuu wa maisha kwa wanaume kuwapenda wanawake wenye umri mkubwa zaidi yao, huku wanawake kupenda wanaume watu wazima. ‎Wito huo umetolewa leo Aprili 30, 2025 na Mkuu wa Wilaya ya Muheza mkoani Tanga, Zainab Abdallah ambaye ndiye aliyekuwa…

Read More

VITUO VYA GESI ASILIA NCHINI SASA NI TISA

          ::::::::  Hadi Aprili, 2025 jumla ya vituo 9 vya CNG vimekamilika na vinatoa huduma, ikilinganishwa na vituo viwili (2) mwaka 2020/21.  Mwelekeo wa Serikali ni kuwa na vituo 7620 ifikapo Juni, 2026.  Aidha EWURA iliendelea kusimamia shughuli za udhibiti katika mkondo wa kati na chini wa gesi asilia kwa kufanya…

Read More

SMZ yapokea vifaa vya Sh1.9 bilioni vya kuhifadhia taka

Unguja. Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) imepokea vifaa vya kuhifadhi na kusafirishia taka ngumu vyenye thamani ya Sh1.9billioni kupitia mradi wa Ukuzaji Uchumi Jumuishi (BIG Z) unaofadhiliwa na Benki ya Dunia. Vifaa ambavyo vimekabidhiwa ni gari za kubebea taka, vikapu na makontena ya kuhifadhia, ambapo hizo ni juhudi za kuimarisha usafi kisiwani hapa.  Akizungumza…

Read More

Rais Samia atoa neno ushirikishwaji sekta binafsi bandarini, mapato yakiongezeka

Unguja. Rais Samia Suluhu Hassan amesema ushirikishwaji wa sekta binafsi katika uendeshaji wa bandari na miundombinu mingine umechangia mafanikio makubwa nchini, ikiwemo ongezeko la mapato. Amesema kati ya Julai hadi Februari mwaka 2024/25, mapato ya bandari na ushuru wa forodha yamefikia Sh8.26 trilioni, ikilinganishwa na Sh7.08 trilioni mwaka 2023/24. Aidha, gharama za uendeshaji wa Bandari…

Read More