Vyombo vya habari vyatakiwa kufichua rushwa uchaguzi mkuu
Dar es Salaam. Vyombo vya habari nchini vimetakiwa kuwa mstari wa mbele katika mapambano dhidi ya rushwa hususani kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu. Hayo yameelezwa na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Crispin Chalamila wakati akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari katika warsha…