Heche ahoji Polisi kuzingira makazi yake na ya Lissu, Kamanda Muliro amshangaa
Dar es Salaam. Wakati John Heche akisema askari Polisi wamezingira makazi yake na ya Tundu Lissu, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro amemshangaa makamu huyo mwenyekiti wa Chadema bara akisema alipaswa kushukuru na kupongeza hatua ya jeshi hilo kumuimarishia ulinzi. Kamanda Muliro amesema Jeshi la Polisi linafanya kazi katika maeneo…