Thamani ya kura yako ni sauti yako, nguvu yako
Nakaribia kutimiza umri wa miaka 60. Tangu uchaguzi wa mwaka 1990 hadi uchaguzi wa mwaka huu, nimepiga kura mara saba na uchaguzi ujao utakuwa wa nane. Kwa zaidi ya miaka 40, nimekuwa nikitimiza wajibu wangu wa kidemokrasia kwa kupiga kura. Hata hivyo, katika kipindi chote hicho, sijawahi kufundishwa wala kuelezwa kwa kina kuhusu thamani halisi…