CAG: Sh2.59 trilioni zilizokusanywa na TRA hazikupelekwa panapohusika
Dar es Salaam. Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) imeeleza kuwa Sh2.59 trilioni ya tozo mbalimbali kilichokusanywa kupitia Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) hazikupelekwa katika taasisi husika. CAG amesema kuwa katika ukaguzi wake kwa mwaka wa fedha 2023/24 ulibaini kuwa jumla ya Sh2.59 trilioni zilikusanywa na TRA kwa niaba ya…