
Wateja wa Benki ya FBME wasotea amana zao miaka saba, waiangukia Serikali
Dar es Salaam. Waliokuwa wateja wa Benki ya FBME zaidi ya 6,000 wameiangukia Serikali wakitaka kuharakishwa kwa mchakato wa malipo ya amana zao zinazodaiwa kuwa zaidi ya Sh31 bilioni wanazodai kwa takribani miaka 7 sasa. Benki hiyo iliwekwa chini ya ufilisi Mei mwaka 2017 baada ya Marekani kuituhumu FBME tawi la Tanzania kuhusika na utakatishaji…