
Mtoto wa Zuma kortini akituhumiwa kuchochea ghasia
Durban. Duduzile Zuma-Sambudla, binti wa Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Jacob Zuma, amefikishwa mahakamani leo Alhamisi Februari 6, 2025 baada ya kushtakiwa kwa kuchochea vurugu wakati wa ghasia za mwaka 2021 ambapo zaidi ya watu 300 waliuawa. Wakili wa Zuma-Sambudla amesema amekana mashitaka hayo. Waendesha mashtaka wanadai kuwa Zuma-Sambudla alichochea watu wengine kufanya vurugu…